Erik Mose ambaye ni mwenyekiti wa tume huru inayochunguza ukiukaji wa haki za binadamu nchini Ukraine amewaambia waandishi wa habari kuwa jopo lake limepata kuwa wanawake kwa wanaume katika mikoa yote ya Ukraine iliyo chini ya udhibiti wa Urusi, wamekuwa wakiteswa.
Mpango wa Umoja wa Mataifa Urusi haukutoa tamko lolote kuhusiana na ripoti ya tume hiyo ya watalaam wa Umoja wa Mataifa.
Uchunguzi Ukraine na ndani ya Urusi
Mose amesema kwamba Ukraine pamoja na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC wanafanya uchunguzi kuhusiana na uwezekano wa kufanyika kwa matukio ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu nchini humo na huenda kama tume wakaitishwa ushahidi.
Mose amesema makamishena wake wamechunguza ripoti kutoka jela 41 tofauti katika maeneo tisa yaliyokaliwa na Urusi nchini Ukraine na maeneo 8 nchini Urusi.
Amesema kwamba tume hiyo imebaini kuwa mateso ambayo hufanywa katika jela za Urusi yanafanywa pia katika jela zilizoko katika maeneo waliyoyakalia nchini Ukraine.
Mose ameongeza kuwa wamepata ushahidi wa ziada wa udhalilishaji wa kingono kutumika mara kwa mara kama njia ya mateso.
Athari za kisaokolojia miongoni mwa wafungwa
Kamishena wa tume hiyo Vrinda Gover amesema wafungwa walibakwa, wakalazimishwa kuketi uchi kwa muda mrefu na kukaguliwa na kufanyiwa mambo mengine mengi zaidi.
Gover amesema wahanga wengi wameripoti kudhalilishwa kingono na kwamba wameathirika kisaikolojia kutokana na mateso hayo.
Kamishena mwengine Pablo de Greiff amewaambia waandishi wa habari kuwa kwa sasa wana ushahidi wa itifaki ya Urusi iliyohusika na uratibu na kuwezesha mateso katika jela na vituo vya kuwazuia wafungwa.