Polisi waingia nyumbani kwa Nabii GeorDavie,wakabidhiwa gari ya Million 30 aliyoitengeneza

Nabii Mkuu Dkt GeorDavie amekabidhi gari moja la mkuu wa kituo cha polisi Tengeru kati ya mawili anayoyatengeneza kwa jeshi la polisi Mkoani Arusha kwa lengo la kupambana na uhalifu nakuimarisha ulinzi huku akitarajia kujenga kituo cha polisi Moivo katika kata ya Sekei Mkoani Arusha

Afisa mnadhimu wa polisi Mkoa Kamishna msaidizi wa polisi Debora Lukololo akimuwakilisha Kamanda wa polisi Mkoani Arusha amesema gari hiyo itasaidia kwa kiwango kikubwa huku akiahidi kuwakilisha salamu za pongez kwa Mkuu wa Jeshi la polisi Nchini kufuatia msaada huo

Mhandisi Godluck Mfinanga akimuwakilisha Nabii Mkuu Dkt GeorDavie amemuambia Mkuu wa wilaya ya Arumeru Amiri Mkalipa kwamba gari hiyo imekamilika kwa silimia mia moja na iko tayar kwa ajil ya kazi na imegharimu million 30 katika matengenezo

 

 

Related Posts