Udumavu unachangia tatizo la kufikiri

Wananchi katika Halmashauri ya wilaya ya Geita wameshauliwa kula chakula kwa kuzingatia Makundi sita ya Lishe Bora ili kuepukana na Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza.

 

Kauri hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Geita , Hashim Komba mara baada ya kuwasili katika shule ya Msingi Bugando iliyopo kata ya Nzera na kuzindua zoezi la lishe Bora ambapo Mamia ya wanafunzi na wananchi wamejitokeza kushiriki katika zoezi hilo ambalo kitaifa hufanyika kila mwaka ifikapo October 30 .

 

” Tunapozungumzia lishe tunazungumzia Mfumo Mzima wa ulaji katika maisha yetu kama kuna jambo ni la muhimu sana bhasi ni lishe na kwanini tunaizungumza leo tunazungumza lishe leo kwa sababu kubwa tatu ya kwanza uhai wa mwanadamu Afya bora ya mwanadamu siri kubwa ipo kwenye namna ambavyo anakula kwenye maisha yake , ” DC. Komba.

 

” Leo tunavyozungumza yako magonjwa mengi ambayo yanawatesa watanzania yako magonjwa mengi ambayo yanatusumbua lakini magonjwa hayo yanachangiwa kwa kiwango kikubwa sana na Mfumo wetu wa ulaji tulio nao ukikosea kula vizuri ukala kwa kujaza tumbo yako madhara utayapata ulaji usiofaa unapelekea magonjwa ya shinikizo la Damu , ulaji usiofaa unatuletea sukari , ulaji usiofaa unatuletea changamoto kwenye Figo, ” DC. Komba.

 

” Leo hii kuna magonjwa yakigonga hodi kwenye nyumba yako ni umasikini na ufukara utakuwa umegonga hodi kukiwa na Mgonjwa wa Pressure huduma ya mgonjwa wa Pressure ni ghali ukiwa na Mgonjwa wa kisukari huduma yake ya matibabu ni ghali ukiwa na mgonjwa mwenye changamoto ya Pressure wakati mwingine anaweza kupelekea kupalalaizi kumhudumia mgojwa ambaye amepalalaizi ni Ghali , ” DC. Komba.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita , Rajabu Magaro amewasihi wananchi wawe tabia ya kujitokeza kwa wingi wanapokuwa wanaadhimisha siku muhimu kama hizi za kutoa elimu kwa wananchi ikiwemo masuala ya lishe Bora ili kuondokana na Changamoto za Udumavu.

Related Posts