Na Mwandishi Wetu Michuzi TV
Ushauri huo umetolewa leo Novemba 1,2024 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa bajaji inayotumia nishati ya umeme wa jua( Solar) kwa wanawake wanufaika wa mradi wa ‘She drive to change’ waliopatiwa mafunzo ya udereva kwa ufadhili kutoka Ujerumani
” Niwapongeze sana shirika la Ladies Joint Forum( NGO), kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Ujerumani kuweza kuwafundisha wanawake 30 udereva na wote na kuwapatia leseni huku mkiangalia namna ya kuwapatia vyombo vya usafiri ili waweze kujiinua kiuchumi mimi naamini mwanamke ndiye mwangalizi wa familia akiwezeshwa anaweza kuinua na wengine” amesema Tabu
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Ladie Joint Forum Francisca Mboya amesema bajaji hiyo iliyozinduliwa wanufaika wa mradi wa She dreve to change ambapo watajipatia kipato na wataendelea kuongeza bajaji nyingine kupitia fedha mbalimbali watakazochangiwa na wadau.
” She drive to change ni mradi wa miezi 12 uliolenga kuwezesha na kukuza.uhuru wa kiuchumi wa wanawake 30 wenye umri wa miaka 18-40 katika kata ya Vingunguti Wilaya ya Ilala Jijini Dar es salaam na unazingatia hasa wahanga walionyanyaswa kijinsia,kina mama vijana walemavu na wale wanaolea watoto wenye ulemavu peke yao” amesema Francisca