SERIKALI YATAKA RIADHA KUAMKA ZANZIBAR,TIGOZANTELI YAPONGEZWA

 MAKAMU wa pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla,
amesema kwa sasa ni zamu ya mchezo wa raidha kuamka na kpanda juu baada ya soka.
Akizungumza kwenye mbio za Kimataifa za ‘Tigo- Zanter Marathon 2024’
zilizofanyika leo asubuhi Zanzibar, Makamu wa pili wa Rais Abdulla, alisema
mchezo wa soka Zanzibar umepiga hatua ambapo kumekuwa na timu nyingi na vijana
wengi wanashiriki hivyo lazima na riadha nao uinuke visiwani humo. “Nawapongeza
waandaaji wa mbio hizi, ni wakati sasa kwa mchezo huu wa riadha kuinula huku
Zanzibar kama ilivyo soka,” alisema. Makamu wa Pili wa Rais alimuwakilishi Rais
wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi na kushiriki
matembezi ya kilometa tano.

Mbio hizo zinazofanyika kwa msimu wa nne mfululizo
zilishirikisha mami ya wakimbiaji kutoka Zanzibar na nje ya Zanzibar. Awali
akizungumzia mbio hizo, Mkuu wa biashara wa Tigo- Zantel, Isaack Nchunda,
alisema wanaamini mbio hizo zimeongeza chachu ya ukuaji wa uchumi visiwani humo.
“Tunaamini mbio hizi zinatupa jukwaa bora zaidi la kutangaza utalii wa Zanzibar,
kukuza vipaji vya wanariadha, kuimarisha afya, na kuchangia katika kuchagiza
uchumi wa bluuhapa visiwani hapa,” alisema Nchunda. Aidha, alisema dhamira ya
kampuni hiyo ni kuendelea kuleta mabadiiko chanya kwenye jamii kwa kuwekeza
kwenye miradi na matukio yanayogusa maisha ya wananchi.

Related Posts