Suhulu ya Wagosi yamchefua Aussems

KOCHA wa Singida Black Stars, Patrick Aussems ameonyesha kutoridhishwa na sare waliyoipata katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union na lengo lao lilikuwa ni kushinda na si kugawana pointi.

Singida ikicheza nyumbani Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar ilitoka suluhu na Wagosi na kushindwa kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, baada ya kufikisha pointi 23 na kuishusha Simba iliyokuwa ya pili na alama zao 22. Kama ingeshinda ingefikisha pointi 25 na kuiengua Yanga yenye 24 kwa sasa.

Aussems ameeleza changamoto mbalimbali zilizoikumba timu yake na mikakati ya kuhakikisha wanajipanga upya kabla ya michezo ijayo ya ligi dhidi ya Tabora United, Azam na Simba.

“Tulikuwa na malengo ya kushinda, kugawana pointi hakukuwa kwenye mipango yetu,” alisema Aussems.

Alibainisha timu hiyo ilishindwa kutumia nafasi vizuri walizopata eneo la hatari, jambo aliloliona kama changamoto kuu iliyowazuia kushinda.

Alisema kipindi cha pili, wachezaji walionekana kuwa na haraka katika baadhi ya nyakati, hali iliyosababisha makosa  aliyoyaita ya kijinga, yakiwemo kupoteza mipira na kutopiga pasi kwa usahihi.

“Tulikuwa na hali ya haraka sana kipindi cha pili, jambo lililosababisha kufanya makosa madogo ambayo yaliathiri uchezaji wetu kwa ujumla,” alisema Aussems na kuongeza atatumia mapumziko ya ligi kuopihs akalenda ya mechi za kimataifa za Fifa kujiweka sawa ili warudi na kasi mpya.

Related Posts