TFS WATUMIA MICHEZO KUHAMASISHA JAMII KUHIFADHI MISITU


Wakala wa Uhifadhi wa Misitu Nchini (TFS) wameeandaa bonanza la michezo lenye lengo la kujenga mahusiano, ushirikiano na kuhamasisha jamii katika uhifadhi wa misitu ambalo limewakutanisha washiriki zaidi ya mia mbili (250) kutoka katika kanda nane za Uhifadhi nchini.

Akizungumza wakati akizindua bonanza hilo Jijini Arusha KamshinaMsaidizi Mwandamizi wa TFS CPA (T) Peter Mwakosya akimwakilisha kamishna wa Uhifadhi wa misitu nchini amesema washiriki wametoka katika kanda zote nane na wanashiriki michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,mikono pamoja na riadha.

“Nipende kuelekeza katika kila kanda kutenga bajeti ambazo zitaweza kuwezesha shughuli za michezo kwa askari wetu wa uhifadhi ikiwa ni njia pekee ya kuendelea kuimarisha afya kwa askari wetu” Aliongezea

Kwa upande wake Mratibu wa bonanza hilo Afisa Muhifadhi Mwandamizi kutoka TFS Marcel Bitulo ameeleza kuwa bonanza hilo litatumika katika kuandaatimu ambayo itawawakilisha kwenye mashindano ya SHIMUTA yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi novemba mkoani Tanga.

Ramia Konyo ni mmoja ya wawakilishi wa baadhi ya kanda ambapo amepongeza hatua hiyo na kudai ina tija kubwa katika kuongeza ufanisi katika utendaji kati wao ambao utaongeza umoja na ushirikiano wa watumishi sambamba na kujenga afya zao mahala pa kazi.

Hata hivyo Meneja Uhusiano kutoka TFS Johari Kachwamba ameeleza kuwa mashindano hayo yanalengo la kujenga mahusiano mazuri kwa wafanyakazi wa TFS kutoka katika kanda zote za Tanzania na kuhamasisha watumishi hao kuwa na tabia ya kufanya mazoezi.

Mashindano haya yanafanyika kwa mara ya kwanza kwa kushirikisha kanda zote nane ambazo ni shamba la miti SAOHIL,nyanda za juu kusini,kanda ya mashariki,kanda ya kati,kanda ya kaskazini,kanda ya ziwa pamoja na kanda ya magharibi.










Related Posts