Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limechangia kiasi cha shilingi milioni 50 kwa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa lengo la kusaidia watoto wenye uhitaji wa Matibabu ya moyo.
TPDC imechangia fedha hizo kwenye hafla ya uchangishaji fedha kusaidia watoto 1500 wenye matatizo ya moyo.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Tukio hilo limefanyika leo tarehe 02.11.2024 , Johari Rotana Jijini Dar es salaam.