Halmashauri ya Ifakara Mji kutoa Mikopo yenye thamani ya shilingi Milioni mia Tisa kwa robo mwaka .

Halmashauri ya Wilaya ya Ifakara Mji iliyopo Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro imetenga zaidi ya shilingi Milioni mia Tisa kwa ajili ya mikopo ya asilimia Kumi ya Wanawake,Walemavu na vijana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ya Ifakara Mji Zahara Michuzi amesema mikopo hiyo isiyo na riba imelenga kuwakomboa kiuchumi makundi hayo kuacha kuwa tegemezi katika jamii.

Amesema fedha hizo ni kwa awamu ya kwanza kwa kipindi cha robo mwaka ya kwanza mwaka wa fedha 2024/2025 na kwamba vikundi vyote vyenye vigezo katika Halmashauri hiyo vitapatiwa bila upendeleo wowote.

Michuzi ametoa Wito Kwa makundi hayo kutumia mikopo hiyo vizuri Ili waweze kurejesha na kuwainua kiuchumi kama dhamira ya Serikali.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri hiyo ya Ifakara Mji Frolence Mwambene amesema tangu kuanza kurudishwa Kwa mikopo hiyo hadi Sasa vikundi 170 tayari vimeomba mikopo kupitia mfumo maalum.

Aidha amewataka vijana ,wanawake na Walemavu kuchangamkia fursa hiyo ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa kipindi kirefu .

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa Ifakara wamesema kwa Sasa mikopo hiyo itasaidia kwenye biashara mbalimbali kutokana na kuwepo na barabara ya lami kutoka katika mji huo hadi Jiji Dar es Salam tofauti na zamani .

Wanasema kipindi cha nyuma walikua wakikopa.mikopo lakini kutokana na changamoto ya usafiri biashara zilikuwa zinaharibika wanaishukuru Serikali kwa kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji.

Related Posts