KATIBU MKUU WA CCM AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CRC

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi amekutana na Mheshimiwa Youssoufa Mohamed Ali,Waziri wa Ulinzi ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Tawala Comoro cha CRC ambaye pia ni Katibu wa Rais wa Umoja wa Visiwa vya Comoro na kuzungumzia kuimarisha uhusiano baina ya vyama hivyo ikiwa ni pamoja na kutoa fursa za mafunzo kwa watendaji wa Chama cha CRC nchini Tanzania.
Aidha viongozi hao wamepongeza juhudi za ushirikiano wa nchi hizo mbili unaofanywa na Marais wake Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Azali Assoumani.
Ziara hiyo imeratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro,Mheshimiwa Youssoufa anatarajiwa pia kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete,Shirika la Uzalishaji Mali SUMA JKT na pia Taasisi binafsi kadhaa zenye dhamira ya kuwekeza nchini Comoro.

Related Posts