Mtandao kuunganisha vituo vya ubunifu waanzishwa

Mwenyekiti wa mtandao wa wa Vitovu Tanzania  (THN) Kiko Kiwanga Akizungumza na wadau mbali mbali wa bunifu wakati wa uzinduzi wa mtandao wa kuunganisha na kuimarisha vituo vya ubunifu kote nchini kwa lengo la kuboresha huduma za ubunifu na uvumbuzi sambamba na kuongeza tija.uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 4,2024 Jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Mpango wa Ufunguo, Joseph Manirakiza

Akizungumza na wadau mbali mbali wa bunifu wakati wa uzinduzi wa mtandao wa kuunganisha na kuimarisha vituo vya ubunifu kote nchini kwa lengo la kuboresha huduma za ubunifu na uvumbuzi sambamba na kuongeza tija.uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 4,2024 Jijini Dar es Salaam.

Picha ya pamoja

Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MTANDAO wa Vitovu Tanzania (THN) umeanzisha mtandao wa kuunganisha na kuimarisha vituo vya ubunifu kote nchini kwa lengo la kuboresha huduma za ubunifu na uvumbuzi sambamba na kuongeza tija.

Kuanzishwa kwa mtandao huo kunatajwa kuchochea ujasiriamali na maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania

Akizungumza leo Dar es Salaam, Mwenyekiti wa THN, Kiko Kiwanga amesema hatua hiyo inatoa fursa ya kipekee kwa vituo vya ubunifu nchini Tanzania kuendeleza zaidi ubunifu na ujasiriamali wa nchi.

Amesema kupitia mtandao huo, wanaweza kuwasaidia wabunifu kwa ufanisi zaidi, kuboresha huduma wanazotoa, na kuinua taswira ya Tanzania katika mfumo wa ubunifu wa Afrika.

Pia ameeleza kuwa wanahudumia wajasiriamali na wabunifu wa teknolojia, dijitali na ule ubunifu wa kawaida kutoka katika jamii.

“Tunalenga kujengea uwezo vituo vya ubunifu, kutengeneza mfumo wa ubunifu ili kutoa huduma imara za ubunifu,” ameeleza.

Pia amewataka wadau kuendelea kushirikiana nao kuinua vituo hivyo viweze kutoa huduma bora.

Amesema kwa kushirikiana na FUNGUO Innovation Programme, mpango wa UNDP Tanzania unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya na Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza na Maendeleo ya Jumuiya (FCDO), THN inaleta pamoja zaidi ya vituo vya ubunifu 35 vyenye dhamira ya pamoja ya kutoa msaada wa kina kwa wajasiriamali na wabunifu, hususan katika teknolojia.

“THN inatoa jukwaa la kipekee kwa vituo vya ubunifu nchini Tanzania kuboresha mchango wao na kuunda mtiririko wa mradi unaochochea mazingira ya ubunifu kitaifa,” amesisitiza.

Meneja wa Mpango wa Ufunguo, Joseph Manirakiza anaeleza kuwa ili kuimarisha zaidi uwezo wa ubunifu nchini Tanzania, mpango huo unaoungwa mkono na UNDP unafadhili mameneja wa vituo 15 kutoka Tanzania kuhudhuria Mkutano wa Afrilabs Annual Gathering (AAG) 2024 huko Cape Town, Afrika Kusini.

Amesema fursa hiyo inayofadhiliwa kikamilifu inawapa mameneja wa vituo nafasi ya kujifunza kutoka kwa viongozi wa ubunifu wa Afrika, kupata maarifa ya kimataifa, na kuunda ushirikiano wa kimkakati utakaowasaidia wabunifu wa Kitanzania kusaidia kampuni changa na suluhisho zenye tija na ubunifu.

“Kwa kuanzisha Tanzania Hubs Network, tunaweka msingi wa mfumo wa ubunifu wenye mshikamano na uimara. Ufadhili wetu kwa mameneja wa vituo kuhudhuria Mkutano wa Afrilabs ni uwekezaji wa kimkakati unaowezesha vituo vya ubunifu vya Tanzania kujifunza, kushirikiana, na kurudisha utaalamu muhimu utakaowasaidia wajasiriamali wetu wa ndani,” ameeleza.

Pia ameushukuru Umoja wa Ulaya na Serikali ya Uingereza, pameoja na serikali ya Tanzania kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kwa msaada wao mkubwa ambao ni chachu ya kufanikisha maono hayo.

Naye, Rachel Magodi kutoka Ifakara Innovation Hub, amesema fursa ya kuwa na mahusiano na Mataifa mengine kuendana na huduma anazotoa kukuza ujasiriamali na ubunifu Tanzania.

Amesema watakaporudi wataboresha huduma na utawala wa vituo kuwa na tija.

Related Posts