Rais Mwinyi awasili nchini China

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi akimbatana na Mke wake Mhe. Mama Mariam Mwinyi amewasili katika uwanja wa ndege wa Pudong International Airport, Shanghai, China akitokea Doha, Qatar na kupokelewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, China Mhe. Khamis Mussa Omar.

Rais Dk. Mwinyi na ujumbe wake wanatarajiwa kuhudhuria ufunguzi wa Maonesho ya 7 ya China International Import Expo (CIIE) pamoja na kutembelea mabanda ya washiriki mbalimbali ya maonesho hayo.

Aidha, katika maonesho hayo Tanzania imepewa heshima maalum kuwakilisha bara la Afrika kutokana na mchango mkubwa wa zaidi ya Kampuni 17 pamoja na sekta za kilimo, kazi za sanaa za mikono, bidhaa za kilimo na uchumi wa buluu.

Related Posts