Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti kitita cha Mil.6 ambayo sehemu ya mchango wake kwenye Kisarawe Afya Gala.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika tarehe 2, Novemba ,2024 kwenye Ukumbi wa Minaki Sekondari.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali.
Na Khadija Kalili Michuzi Tv
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Mhe.Petro Magoti ameongoza harambee ya uchangishaji wa fedha za ujenzi wa jengo la VIP Hospitali ya Kisarawe Mkoani Pwani.
Hafla hiyi imefahamika kama Kisarawe Afya Gala ilinefanyika tarehe2, Novemba,2023 kwenye Ukumbi wa Sekondari ya Minaki.
Kwenye hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti
ametembeza bakuli meza baada ya meza kwa wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo ikiwa ni katika kuchangia ujenzi wa jengo la wagonjwa la VIP Hospitali ya Kisarawe Mkoani Pwani.
DC Magoti amesema kuwa wamefanikiwa kukusanya fedha taslimu kiasi cha Ml.100 jambo ambalo linaonesha taswira nzuri katika kufikia lengo la ujenzi jengo jipya na la kisasa linalokadiriwa kugharimu kiasi cha Mil.250 hadi kukamilika.
Aidha mgeni rasmi kwenye hafla hiyo alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti akizungumza kuhusu tathmini ya hafla hiyo amesema kuwa wamepata kiasi cha Mil.100 ambazo wataanza ujenzi wa jengo hilo mara moja.
“Tulikuwa tunahitaji kiasi cha Mi.200 lakini tumepata Mil.100 si haba hivyo tutaanza ujenzi na pindi zitakapoisha tutaitisha harambee ingine ya kuchangia umaliziaji wa jengo hilo” amesema DC Magoti.
Wakati huohuo amesema kuwa wanapokea misaada ya vifaa vya ujenzi ikiwa ni pamoja na mabati,saruji,kokoto michaga na vifaa vyote vinavyohitajika kwenye ujenzi.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Waziri Jafo amesema kuwa anaishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na waratibu wengine kwa kuratibu tukio hilo muhimu pia amefurahi kuona Waalimu wa ngazi za chini kwa namna walivyojitokeza kwa wingi huku akisisitiza kuwa kuna mambo mbalibali ambayo yanahitaji nguvu ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuchangishana katika ujenzi wa nyumba za waalimu huku akisema kuwa milango iko wazi kwa kila mdau kwa sababu lengo ni kuijenga Kisarawe.