Ujerumani inaweza kukabiliwa na uchaguzi wa mapema – DW – 04.11.2024

Waziri wa Fedha wa Ujerumani Christian Lindner ameibua mvutano mpya ambao wachambuzi wanakubaliana kwamba unaiweka serikali ya Ujerumani ya mrengo wa kushoto-kati katika hatari ya kuporomoka.

Lindner ambaye ni mwenyekiti wa chama cha kiliberali Free Democrats (FDP) ameandika kurasa 18 za mapendekezo ya kile anachokiita “mabadiliko ya kiuchumi na marekebisho ya kimsingi ya maamuzi muhimu ya kisiasa”.

Miongoni mwa mapendekezo hayo yakiwa ni kupunguza kodi kwa makampuni, kuzingatia upya sheria za kukabili mabadiliko ya tabia nchi na kupunguza misaada ya kijamii.

Mapendekezo hayo hayaambatani na vyama vinavyoshirikiana katika serikali hiyo ya muungano, hususan chama chake Olaf Scholz (SPD) na chama cha watetezi wa mazingira . KUmekuwa na ukosoaji mkali dhidi ya hatua hiyo ya Lindner.

Lindner amesema, taarifa hiyo haikukusudiwa kutolewa kwa umma.

Je kansela ajaye wa Ujerumani ataweza kuleta mabadiliko Afrika?

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Soma pia:Hakuna Imani!: Muungano tawala Ujerumani waendelea kuwa njiapanda

Mjadala huo unaibuka wiki moja tu kabla ya makadirio ya bajeti ya mwaka 2025 kuwasilishwa. Chama cha upinzani cha kihafidhina tayari kinaitisha uchaguzi wa mapema.

Chaguzi kuu za Ujerumani hufanyika kila baada ya miaka minne na uchaguzi mkuu ujao umepangwa kufanyika Septemba 2025.

Lakini uchaguzi wa mapema unaweza kuandaliwa kukiwa na mgogoro wa kisiasa, mfano ikiwa mkuu wa serikali, amepoteza uungwaji mkono bungeni.

Chaguzi hizo za mapema ni nadra sana nchini Ujerumani, lakini ni hatua muhimu za kidemokrasia. Zinadhibitiwa na katiba ya Ujerumani na ili zifanyike, ni sharti ziidhinishwe na asasi za kikatiba akiwemo rais.

Mambo mawili yanayoweza kutokea

Kulingana na katiba ya Ujerumani, uamuzi wa kufanya uchaguzi wa mapema wa shirikisho, hauwezi kufanywa na wajumbe wa bunge la chini Bundestag, wala na kansela. Bunge la shirikisho linaweza kuvunjwa mapema tu ikiwa moja kati ya mambo haya yatatokea.

SPD | Ujerumani | Kansela Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Jens Schlueter/Pool Photo/AP/picture alliance

Kwanza, ni ikiwa mgombea wa ukansela hatashinda wingi unaohitajika bungeni, ambayo ni viti visivyopungua 367 kati ya jumla ya viti 733 katika bunge la shirikisho- Bundestag.

Katika hali hiyo, rais wa Ujerumani atalivunja bunge. Tukio kama hili halijawahi kutokea katika historia ya jamhuri ya Ujerumani.

Pili ni ikiwa kansela ataitisha kura ya imani bungeni kuthibitisha ikiwa angali na uungwaji mkono wa bunge au la.

Soma pia:Chama cha SPD chapata ushindi uchaguzi wa Brandenburg

Ikiwa atashindwa kupata wingi unaohitajiwa wa wabunge, basi anaweza kumuomba rasmi rais kulivunja bunge ndani ya siku 21.

Baada ya bunge kuvunjwa, chaguzi mpya ni sharti zifanyike ndani ya siku 60. Zinaandaliwa kwa njia kawaida kama chaguzi kuu

Hadi sasa chaguzi tatu za mapema za bunge zimewahi kufanyika katika Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani: Nazo ni mnamo 1972, 1983 na 2005.

Hili si jambo geni kwa Ujerumani

Willy Brandt, kansela wa kwanza wa Ujerumani kutoka chama cha Social Democratic (SPD), aliongoza serikali y amuungano na chama cha Free Democratic (FDP) kuanzia mwaka 1969.

Lakini siasa zake za kuegemea Mashariki zilichochea kura ya Imani mnamo mwaka 1972. Katika kura hiyo Brandt pande zote pinzani zilipata kura sawa 248.

Hali ya mkwamo ulipoibuka, Brandt aliitisha kura ya Imani mnamo Septemba 20 na akashindwa kama tu alivyopanga.

Hali hiyo ilisababisha bunge kuvunjwa na uchaguzi mpya kufanywa.

Helmut Kohl, wa CDU, alihusika katika uchaguzi wa mapema wa 1983. Alichukua mamlaka baada ya kura ya Imani iliyomuondoa kansela Helmut Schmidt wa SPD mnamo Oktoba 1982 kufuatia tofauti kuhusu sera zake za kiuchumi na kisiasa.

Wapiga kura wa mara ya kwanza hawafurahii matokeo ya uchaguzi

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Soma pia:AfD na matumaini ya kushinda uchaguzi wa jimbo la Brandenburg

Naye Gerhard Schröder wa SPD alisababisha uchaguzi wa mapema wa tatu mnamo mwaka 2005 alipokuwa kansela wa wakati huo akiongoza serikali ya muungano na chama cha watetezi wa mazingira.

Chama chake SPD kilikuwa kikiyumbayumba baada ya misururu ya matokeo mabaya na uungwaji wake mkono bungeni ulizidi kupungua.

Hasa kutokana na ajenda yake tete ya mageuzi ya mwaka 2010, ambayo yalibadilisha pakubwa mfumo wa kijamii na soko la ajira.

Schröder aliitisha kura ya Imani ambayo alishindwa Julai mosi 2005 na kuchochea uchaguzi mpya.

 

Related Posts