Habari Vodacom Tanzania na UDSM Zaungana Kuwezesha Kizazi Kijacho cha Wataalamu wa Usalama wa Mtandao (Cyber Security Experts). November 4, 2024 Admin Mkuu wa Idara ya Usalama wa Mtandaoni kutoka Vodacom Tanzania Plc Bw. Joel Kazoba akizungumza katika uzinduzi wa klabu ya usalama wa mitandao uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha Tehama kilichopo Kijitonyama. Klabu hiyo imezinduliwa kwa ushirikiano baina ya Vodacom na chuo hicho cha Tehama yenye madhumuni ya kuhamasisha wanafunzi kujiunga katika masomo ya usalama mtandaoni na kuwapa uzoefu wa vitendo katika kukabiliana na vitisho vya usalama wa kidijitali. Pembeni ni Mkuu wa Kitengo cha mafunzo ya kielectroniki Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Baraka Maiseli. Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bi. Warda Obathany (Kushoto) akimkabidhi cheti mshindi wa kwanza mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam cha Tehama Alexus Samson (Kulia) wa michezo ya vitendo maarufu kama “capture the flag”. wa mashindano ya kudukua mifumo (capture the flag) Mashindano hayo yalifanyika katika uzinduzi wa klabu ya usalama Chuoni hapo wiki hii. Uzinduzi huo ulifanywa na Vodacom Tanzania plc kwa kushirikiana na chuo cha Tehama UDSM klabu hii inaenda kuhamasisha wanafunzi kujiunga katika masomo ya usalama mtandaoni na kuwapa uzoefu wa vitendo katika kukabiliana na vitisho vya usalama wa kidijitali. Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bi. Warda Obathany (Kushoto) akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam cha Tehama UDSM Rafia Maganga (Kulia) wa mashindano ya kudukua mifumo (capture the flag) Mashindano hayo yaliofanyika katika uzinduzi wa klabu chuoni hapo wiki hii. Uzinduzi huo ulifanywa na Vodacom Tanzania plc kwa kushirikiana na chuo cha Tehama UDSM klabu hii inaenda kuhamasisha wanafunzi kujiunga katika masomo ya usalama mtandaoni na kuwapa uzoefu wa vitendo katika kukabiliana na vitisho vya usalama wa kidijitali. Related Posts Habari MUFTI MKUU TANZANIA KUJA NA ZIARA YA KUIMARISHA UONGOZI MKOA WA DODOMA January 19, 2025 Admin Habari Chadema yapitisha 23 kuwania ujumbe Kamati Kuu January 19, 2025 Admin