Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania Bw. Nguvu Kamando akizungumza na wanavikundi vya VICOBA katika hafla ya kusheherekea siku ya VICOBA iliyofanyika Alhamisi tarehe 31 Oktoba katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Vodacom walitumia hafla hiyo kuzindua vifurushi vya bei nafuu maalumu kwaajili ya vikundi hivyo vya kijamii ikiwa ni moja ya adhma yao ya kuhakikisha huduma za mtandao zinawafikia watu wote. Nyuma ni wafanyakazi wa Vodacom Tanzania.