BIL. 250 ZIMETOLEWA NA SERIKALI KWA AJILI YA VIFAA TIBA

Serikali imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 250 katika mwaka wa fedha 2024/25 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwa maeneo yote ya kutolea huduma za Afya ya msingi katika Halmashauri zote 184 nchini.

Taarifa hiyo imetolewa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati akijibu swali la Dkt. Pius Chaya ,mbunge wa jimbo la Manyoni mashariki aliyetaka kujua mpango wa serikali wa kupeleka jokofu la kuhifadhia maiti katika kituo cha Afya cha Nkonko.

Akijibu sawali hilo Mhe. Dkt. Dugange amemuelekeza mkurugenzi wa Halmadhauri ya Manyoni mkoa wa Singida kuweka kipaumbele cha ununuzi wa Jokofu katika kituo hicho cha Afya ili wananchi wapate huduma hiyo.

Aidha,Akijibu swali la pili la Mhe. Dkt. Chaya linalohusu serikali kujenga wa vituo vya Afya vya kimkakati nchini katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/25, Dkt. Dugange amesema serikali iko katika hatua za mwisho za kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa vituo vya kimkakati katika majimbo yote 214 nchini.

“Serikali ishatoa taarifa na maamuzi ambayo kupitia Rais wetu mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa majimbo yote 214 yatakwenda kujengewa vituo vya Afya na tayari tuko hatua za mwisho za kutoa fedha kwaajili ya kwenda kujenga vituo hivyo vya Afya lakini kuna majimbo 18 ambayo mpaka sasa hatujapata mapendekezo ya kata ambazo wanahitaji kujenga vituo vya Afya” Amesema

Related Posts