Dk Manguruwe afikishwa mahakamani, asomewa mashtaka 28

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla International Ltd, Simon Mkondya (40) maarufu kwa jina la Dk Manguruwe na mkaguzi wa kampuni hiyo, Rweyemamu John (59) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka 28 yakiwamo ya kuendesha biashara ya upatu na kutakatisha fedha, kinyume cha sheria.

Washitakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo, leo Jumanne, Novemba 5, 2024 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi namba 31523 ya mwaka 2024.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Job Mrema amewasomea mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya.

 Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts