Na Jane Edward, Arusha
Ameyasema hayo katika mkutano wa Tatu wa Makamanda wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) uliofanyika leo Novemba 5, 2024 kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha.
“Upo ushahidi kabisa kwamba matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA inasaidia kuboresha kazi, utawala bora na kupunguza vitendo vya rushwa ambavyo vingeweza kujitokeza, kuimarisha makusanyo na kudhibiti matumizi ya maduhuli ya serikali” Mhe. Chana amesisitiza.
Amewataka Wahifadhi hao kuweka nguvu kwenye kuzuia uhalifu, uharibifu, kutoa elimu, mafunzo na kuweka mabango yanayoonekana katika maeneo ya misitu yaliyohifadhiwa hasa kwa kutumia mbinu na vifaa vya za kisasa.
“Endeleeni kuimarisha ulinzi wa misitu hii kwa kuhakikisha misitu yote inajengwa vituo vya ulinzi hususan sasa na matumizi ya Teknolojia katika ulinzi ambapo changamoto za uhifadhi zinaongezeka, kama kutumia ndege nyuki na satellite” Mhe. Chana amesisitiza.
Katika hatua nyingine, Mhe. Chana amewataka wahifadhi hao kufanya kazi kwa uadilifu, weledi wenye mbinu za kijeshi kwa kuzingatia masuala ya haki jinai.
Amewataka kutumia fursa za ukuaji wa utalii nchini kuendeleza utalii wa misitu (Forest Based Tourism) na kusisitiza kuwa fursa hiyo ikitumika vizuri itatoa mchango mkubwa katika uhifadhi na kukuza kipato cha jamii na taifa.
Amefafanua kuwa pamoja na mambo mengine kikao hicho kitatoa mada kuhusu Intelijensia ya mawazo, fikra za kimkakati, kujenga uwezo wa kuongoza, usimamizi wa sekta ya misitu , mbinu za uongozi, usimamizi wa sera na sekta ya ufugaji nyuki, changamoto na mwelekeo wake.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Washiriki takribani 240 ikijumuisha Viongozi wa Kanda zote Saba za TFS pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya TFS, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Deusdedit Bwoyo, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Menejimenti ya TFS, Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa Mashamba na Wilaya wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).