Mwanamuziki Chuma wa chuma Kizimbani kwa kuishi nchini bila kibali

MWANAMUZIKI Ferdnand Ndikuriyo(27) maarufu kama Chuma wa Chuma amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shtaka moja la kuishi nchini bila kibali.

Chuma ambaye ni Raia wa Burundi anayeishi Mbezi Louis, Dar es Salaam, amesomewa shtaka lake na wakili wa serikali Ezekiel Kibona mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swalo.

Inadaiwa Septemba 18, 2024 huko katika eneo la Upanga, Las Vegas Casino Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam alibainika kuishi nchini bila ya kuwa na kibali wala nyaraka ya kumruhusu kupita ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande. kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika wameomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuja kutajwa.

Aidha Kibona amedai upande wa mashtaka umewasilisha maombi ya kuzuia dhamana ya mshitakiwa huyo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho kwa ajili ya kusikiliza uamuzi juu ya ombi hilo la kupinga dhamana


Related Posts