Beki wa kushoto wa Simba, Valentin Nouma amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Burkina Faso (The Stallions), kinachojiandaa kucheza michezo miwili ya kufuzu AFCON 2025, huku nyota wa Yanga Stephane Aziz KI akiachwa tofauti na ilivyo zoeleka.
Burkina Faso itacheza dhidi ya Senegal Novemba 14, kwenye Uwanja wa Stade du 26 Mars na Novemba 14 ikiwa ugenini itacheza dhidi ya Malawi kwenye Uwanja wa Bingu.
Katika kundi L la kufuzu Afcon 2025, Burkinafaso ndiyo inayoongoza kundi ikiwa na pointi 10 sawa na Senegal inayoshika nafasi ya pili, zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa, huku namba tatu ni Burundi yenye pointi tatu na Malawi ikishika mkia ikiwa haijapata pointi katika mechi nne ilizocheza.
Hata hivyo tayari Burkinafaso na Senegal tayari zimeshafuzu AFCON 2025, zitakazofanyika Morocco.
Kikosi kilichoitwa na Kocha Brama Traore
MAKIPA
Herve Koffi, Farid Ouedraogo na Kilian NIKIEMA
MABEKI
Issa KABORE, Steeve YAGO, Edmond TAPSOBA, Nasser DJIGA, Valentin NOUMA, Mohamed OUEDRAOGO, Issouf DAYO na Trova BONI
VIUNGO
Sacha BANSE, Cedric BADOLO, Saidou SIMPORE, Blati TOURE, Dramane SALOU, Kader OUATTARA, Ousseni BOUDA na Gustavo SANGARE
WASHAMBULIAJI
Ousmane CAMARA, Bertrand TRAORE, Hassane BANDE, Dango OUATTARA, Franck Lassina TRAORE na Mohamed KONAT