POLISI imeonyesha ubabe wake kwenye Ligi ya Kikapu Divisheni 1 baada ya kuichapa Stein Warrious kwa pointi 71-58, kwenye Uwanja wa Donbosco Oysterbay.
Katika mchezo huo, ulikuwa na ushindani mkubwa kama fainali na Stein ilianza robo ya kwanza kwa uweleano mkubwa, huku Polisi ikionekana kucheza taratibu.
Hadi robo hiyo inamalizika Stein ilikuwa mbele kwa pointi 16-14, kabla ya robo ya pili Polisi kuongoza kwa pointi 21-19.
Robo ya tatu Polisi ilianza mchezo kwa kuipeleka putaStein na kupata pointi 19-11 na 17-12.
Katika mchezo huo, Siaba Saidi alifunga pointi 29, akifuatiwa na Faham Hamadi na Law Mwambasi waliofunga pointi 21 na 14.
Upande wa Stein James Ngaboeka alifunga pointi 11, akifuatiwa na Mwinyi Pemba aliyefunga nane.