Sakata la Engonga kuhusishwa na video za ngono lachukua sura mpya

Dar es Salaam. Serikali ya Guinea ya Ikweta imeanza kuweka vikwazo kwa matumizi ya mtandao wa WhatsApp nchini humo, ikilenga kuzuia raia kupakua na kusambaza picha na video zinazohusiana na kashfa ya ngono inayomhusisha Baltasar Engonga, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika  wa Fedha.

Engonga anatuhumiwa kujirekodi akijihusisha na vitendo vya ngono na zaidi ya wanawake 400, wakiwemo wake wa maofisa wa serikali, katika ofisi na nyumbani kwake.

Hatua hiyo ya serikali imesababisha hasira kwa watumiaji wa WhatsApp, wakieleza kuwa matendo ya wachache yamevuruga shughuli zao za kila siku kwenye mtandao huo.

Kashfa hiyo iligundulika baada ya polisi kufanya upekuzi nyumbani na ofisini kwa Engonga, kufuatia uchunguzi wa madai ya ufisadi na udanganyifu.

Wakati wa upekuzi huo, mamlaka zilipata kanda kadhaa zenye video za wanawake hao zaidi ya 400, wakiwemo wake za viongozi, mke wa mchungaji wa Engonga, jamaa wa rais wa nchi hiyo, na wake za mawaziri zaidi ya 20.

Ikumbukwe Makamu wa Rais wa Guinea ya Ikweta, Teodoro Nguema jana alitangaza kuwachukulia hatua maofisa wote wanaodaiwa kujihusisha na uhusiano wa kingono sehemu za kazi.

Related Posts