Vijana na Wanawake jiungeni kwenye vikundi vya wajasiriamali.

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh Saad Mtambule amewataka wajasiriamali kujiunga kwenye vikundu ili vitambulike na kuviwezesha kupata mikopo ya serikali kwa urahisi ikiwemo kutoka halimashauri.

Mh Saad Mtambule ameyeasema hayo akiwa katika kata ya Bunju wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam wakati akiongea na vikundi vya wajasiriamali zaidi ya 100 huku zoezi hilo likiambatana sambamba na upimwaji wa afya bure kwa wananchi wa maeneo hayo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa vikundi vya wajasiriamali wa Bunju women Bi Jackline Mkina amesema kuwa kuna baadhi ya changamoto zinazo wakabili katika biashara zao nazo ni kupata kiwanja au jengo kwa ajili ya ofisi pia mitaji ya biashara kwa vijana wa eneo la Bunju kwani vijana wanafanya mambo makubwa na wanahitaji mitaji.

Pia changamoto nyingine ni kutokuwa na kituo cha polisi Bunju kwani inapelekea kuhatarisha maisha ya wamama na wakazi wa Bunju ni kilio kwahiyo tunaomba sana kituo kijengwe cha polisi.

 

Related Posts