DAWASA YAINGIA MTAANI TEMEKE,TABATA KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI

Watendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakiongozwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Mkama Bwire imepita katika maeneo ya Temeke na Tabata kuangalia hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa Wananchi na kushuhudia uimarikaji wa huduma katika maeneo ya Soweto, Azimio, Kichangani,Mtongani, Kwa Gude,Lumo, Ikizu Kigilagila, kiwanda Cha vinywaji Pepsi na kiwanda Cha Sigara kwa Temeke, na Bush road makuburi na Tawi la Yanga kwa eneo la Tabata ambayo awali yalikuwa na changamoto ya huduma.

Mamlaka inatoa wito kwa Wananchi wanaopata changamoto za kihuduma kuwasiliana na DAWASA kupitia 0800110064 (Bure) au ujumbe mfupi 0735 202121 (Whatsap tu).


Related Posts