Hatimae msimu wa sita wa show ya Hello Mr right umerejea

Hatimae msimu wa sita wa show ya Hello Mr right umerejea baada ya msimu wa tano kuwa umemalizia huku mgeni wa msimu huu akiwa ni mtangazaji wa EFM na TVE Dr Kumbuka

Shoo hii ni mwendelezo wa tulipoishia msimu wa tano ambako, Hello Mr Right ilikuwa inaongozwa na Mc Garab akiwa sambamba na Aaliyah Mohamed kama washereheshaji na

watangazaji wa shoo hii, huku Lulu Diva akiwa kama daktari mkali na mshauri wa washiriki. Ila msimu wa sita, ili kuongeza chachu na kuwapa washiriki nafasi ya kusikia uzoefu na ushauri Dr Kumbuka ambaye ana simama kwenye nafasi ya Utetezi wa washiriki haswa waswahili,atakuwa sehemu ya shoo pamoja na wenzake.

Hata hivyo, shoo ya Mr Right Msimu huu itakuwa na mwonekano mpya wa set, huku ikiwa inalenga zaidi kuwa na entertainment kupitia games, Dj Booth pamoja na Photobooth, yenye hadhi ya kisasa.

Hello Mr Right, ina lengo kuwapa nafasi vijana na watu wote wenye umri ambao kwao upo tayari kutafuta mweza wa kujenga nao maisha. Jukwaa hili, limewekwa hususani kwa ajili ya watu wote wenye umri kuanzia miaka 20-45 na kuendelea, ili kuweka bayana uhitaji wao na kupata nafasi ya kukutana na wengine wenye uhitaji huo huo.

Pamoja na hayo yote, pia ni fursa kwa vijana, ambao watapata wachumba, na, wanaweza jipatia vizawadi vidogo vidogo, kwa kadri vinavyopatikana.

Related Posts