Tel Aviv. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na mkewe Sara wamempongeza Donald Trump kwa ushindi wa urais katika uchaguzi mkuu wa Marekani, licha ya kuwa matokeo kamili bado hayajatangazwa.
Netanyau amempongeza Trump pamoja na mkewe Melania leo Jumatano Novemba 6, 2024 kupitia mtandao wa X (zamani Twitter).
“Hongera kwa kurudi tena kwa ubora zaidi katika historia! Kurudi kwako ni kwa kihistoria katika Ikulu, Marekani kunatoa mwanzo mpya kwa Marekani na kujitolea kwa nguvu kwa muungano mkubwa kati ya Israel na Amerika. Huu ni ushindi mkubwa!”
Mwishoni mwa chapisho hilo ameandika “Wako katika urafiki wa kweli,”
Pongezi hizo zinakuja baada ya Trump kuukaribia ushindi kwa kiwango kikubwa na mpaka sasa anaongoza kwa kura 67,341,630 (sawa na asilimia 51.2), wakati Kamala Harris akiwa na kura 62,080,264 (sawa na asilimia 47.4) ya kura zilizohesabiwa mpaka sasa.