Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua rasmi mfuko wa mikopo wenye kianzio cha shilingi bilioni 2.3 kwajili ya kusaidia ubidhaisha na ubiasharishaji wa bunifu na Teknolojia iznazobuniwa na vijana wa Kitanzania katika Kongama o la STICE 2024.
Hayo yameelezwa na Waziri Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu hilo la stice 2024 liliandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Na kuongeza kuwa pia atakabidhi hundreds yenye thamani ya shilingi bilioni 6.3 kwa watafiti 19 katika masuala ya mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo nishati safi ya kupikia.
“Serikali inatarajia kuzindua rasmi mfuko wa mikopo wenye kianzio cha bilioni 2.3 kwa ajili ya kusaidia ubidhaishaji na ubiasharishaji kwa wabunifu na teknolojia zinazobuniwa na vijana wa kitanzania”.
” Kongamano hilo limepangwa kufanyika Desemba mbili hadi Nne jijini Dar es salaam,Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua mfuko huo,pamoja na kukabidhi hundi yenye thamani ya sh bilioni 6.3 kwa watafiti 19,katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi,ikiwemo nishati safi ya kupikia.
Aidha Profesa Mkenda amesema Rais siku hiyo,atawatambua na kutoa tuzo maalum kwa wanasayansi na wabunifu ambao matokeo ya kazi yao,yamechangia kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii ndani na nje ya nchi.
Aidha amesema ni imani yao kuwa kupitia kongamano hilo serikali itapata michango ya kisera na kitaaluma ambayo itasaidia kuimarisha sera mikakati na juhudi nyingine zinazolenga kuimarisha mchango na mshikamano baina ya taasisi,sekta binafsi na wadau wamaendeleo katika kuendeleza STU kama nyenzo kuu ya kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watanzania.
Aidha ameishkuru timu nzima ya maandalizi ya kongamano hilo na kuongeza kuwa Stice ya mwaka huu itakuwa ni hatua nyingine muhimu katika safari yetu ya kujenga taifa linaloongozwa na Sayansi,teknolojia na ubunifu.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH DK Amos Nungu amesema kuwa lengo kubwa la kongamano hilo ni kuwakutanisha wadau mbalimbali kujadili mambo mbalimbali yanayohusu sayansi na teknolojia ikiwemo kuonyesha mambo wanayoyafanya wabunifu.
Na kuongeza kuwa Oktoba Nne mwaka huu walizindua mwongozo wa kitaifa wa masuala ya ubunifu ili uweze kufikiwa na kusaidia kila aina ya ubunifu unaofanywa na wabunifu.
Amesema muongozo huo pia una mtaala mpya ambao utaweza kuwasaidia wanafunzi wenye vipaji tokea ngazi ya chini ambao watapata msaada moja kwa moja kwenda kwenye ufundi.
“Tunaishkuru sana serikali na wadau mbali mbali wanaounga mkono jitihada za mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia,”alisema DK Nungu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia,Dk Caroline Nombo amesema kuwa imeteuliwa kamati mahususi kwa ajili ya kupitia sera yao ya Sayansi na Teknolojia ya mwaka 1996 ambayo ni ya muda mrefu na hivi sasa Sayansi na teknolojia imebadilika hivyo tunaulazima wa kuhuisha sera hiyo ili iendane na hali ya sayansi na teknolojia iliopo sasa.
Amesema bado wanakusanya mawazo katika makundi mbalimbali ili hapo baadae waweze kuwa na kingamano kubwa la kitaifa ili kuangalia maudhui yanayopaswa kuingia katika sera hiyo.
Kongamano hilo litaongozwa na kauli mbiu inayosema Matumizi ya Sayansi,Teknolojia na ubunifu katika kuhimili changamoto za mabadiliko ya tabia ya Nchi na kuchangia kwenye Uchumi Shindani.