Dar es Salaam. Ugumu wa kuagiza bidhaa mtandaoni, utapeli na usalama mdogo wa malipo ya mteja imeifanya Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania kushirikiana na Kampuni PGI Solutions Limited kuunda suluhisho kwa masoko ya bidhaa mbalimbali nchini.
Ushirikiano huo wenye nia ya kurahisisha na kuboresha uzoefu wa ununuzi kwa wateja wa kwa njia ya mtandao, utawapa fursa ya kununua bidhaa za kielektroniki, mitindo, bidhaa za nyumbani, vipodozi na huduma nyingine ambazo zikipatikana sehemu moja na kwa bei rahisi.
Hayo yamesemwa leo Jumatano, Novemba 6, 2024 jijini Dar es Salaam na Meneja Malipo ya Mtandao na Mifumo ya Kidigitali wa Vodacom, Josephine Mushi wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo.
“Tunashukuru PGI Solution kwa kuleta huduma hii kwa wateja wetu, wateja wetu watapata punguzo la bei kwa kila bidhaa watakayo ichagua,” a,ese,a
Amesema malipo ya wateja yatakuwa salama na kitengo cha huduma kwa wateja kitakuwa tayari kwa kuhakikisha kila mmoja anapata huduma kwa wakati bila kikwazo.
Aidha, Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa PGI solutions, Gillsant Mlaseko amesema ushirikiano baina ya Vodacom Tanzania na punguzo app itawawezesha Watanzania kufurahia punguzo la bei kwa bidhaa na huduma mbalimbali.
“Uzinduzi huu ni mwanzo wa mapinduzi katika ununuzi wa bidhaa na huduma nchini,” amesema.
Mlaseko amesema lengo likiwa kutoa unafuu wa bei kwa wateja wa Vodacom na kuwaunganisha wafanyabiashara na wateja kwa njia rahisi na salama.
Kupitia punguzo hilo, Mlaseko amesema huduma hiyo ndani ya Mpesa App, wateja watafurahia punguzo na ofa maalumu kwa bidhaa na huduma nyingi huku wakitumia Mpesa kufanya malipo ya bidhaa hizo.
Baada ya uzinduzi wa ushirikiano huo Mwananchi imezungumza na baadhi ya wateja wa mtandao huo ili kufahamu ni kwa namna gani watanufaika na huduma hiyo ya kununua bidhaa kwa bei rahisi.
Mwajuma Hamisi, mkazi wa Makumbusho amesem ataangiza bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu hasa kipindi hiki cha kuelekea sikukuu.
“Kama kweli wamezindua huduma hiyo nitaagiza bidhaa mbalimbali hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambapo bidhaa nyingi zinapanda bei kutokana na uhitaji mkubwa wa bidhaa hizo,” amesema Hamisi
Twalibu Waziri, mkazi wa Makumbusho amesema uwepo wa huduma hiyo ya kimtandao itamsaidia kuagiza bidhaa za kilektronia.
“Mara nyingi huwa nakwenda kununua bidhaa hizi mwenyewe na huwa nazunguka sana kupata kwa bei nafuu, huwa natamani sana niwe na pata machimbo ya bidhaa hizi kwa bei nzuri ili nipate faida ila kama kunahuduma hii mpya nitaanza kufaidika kwa kuagiza,” amesema.