AIRTEL WAZINDUA DUKA KATIKA KITUO CHA TRENI YA SASA DAR

Mtendaji Mkuu wa TRC, Masanja Kadongosa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la Airtel katika kituo cha Treni ya Kisasa kilichopo jijini Dar es Salaam, leo Novemba 07, 2024.

Mkurungezi wa Mawasiliano kutoka kampuni ya Artel Tanzania Beatrice Singano akifafanua jambo leo mara baada ya uzinduzi wa duka katika kituo cha Treli ya Kisasa jijini Dar es Salaam leo, Novemba 07, 2024.

KATIKA kuthibitisha kuwa Kampuni ya Airtel Tanzania inawathamini wateja wake kampuni oyih imezindua duka jipya katika kituo cha Treni ya Kisasa kilichopo chini ya Shirika la Reli Tanzania(TRC).

Akizungumza na waandishi wa habari wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Novemba 07, 2024 wakati wa uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Airtel Tanzania, Eliud Betri Sanga amesema kuwa duka lililozinduliwa leo ni la 44 hapa nchini.

Duka hilo linalitamwezesha mteja wao anapokuwa safarini kuwa na uhakika wa kufanya miamala yake mbalimbali ya kutoa na kuweka fedha, kunua simu, kurudisha simu kadi pia kama simu imejifunga anaweza kufunguliwa katika duka hilo.

“Unapokuwa safarini usiwe na wasiwasi wa kupata fedha, weka fedha yako kwenye simu ukifika Dar es Salaam ingia kwenye duka la SGR utaweza kutoa hela zako na kuweza kuendelea na biashara zako.

Kwa Upande wa Mtendaji Mkuu wa TRC, Masanja Kadongosa amesema kuwa huo ni ushirikiano mkubwa kati ya TRC na Airtel kwa wateja wanaweza kukata tiketi ‘online’ na malipo yanafanyika kupitia mtandao wa Aitel.

“Tunafurahi sana ushirikiano wetu na Airtel naamini tutaiongeza zaidi na zaidi, lakini na hata ile kuamua kuja kuwekeza katika jengo letu hili ni kitu kinachoongeza thamani kwetu sisi kama TRC.”

Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa wateja wa Kampuni ya Airtel Tanzani, Adriana Liamba amesema kuwa lengo la kufungua duka hilo ni kuhudumia wateja wa Mtandao wa Airtel.

Amesema kuwa katika kituo hicho wateja watapata huduma zote zinazotolewa na mtandao huo.

“Airtel imeruhusu kiwango kikubwa cha fedha kuchukua katika duka hili kwa kuweka ama kuchukua fedha kwa sababu huduma ni bora na wengi wanasafiri wanatumia SGA na Mtandao wa Airtel unashika katika maeneo makubwa ya nchi.”

Amesema unaposafiri kwenye treni lengo uwe unapatikana , umepumzika na uko huru kuhisi furaha inavyowezekana.

Related Posts