Kocha wa Maxi, Mpanzu ashushwa Tabora Utd

MABOSI wa wa Tabora United wajanja sana, saa chache kabla ya kikosi hicho kukabiliana na Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara, mapema tu imeshamshusha kocha aliyewahi kuwanoa nyota kadhaa wanaotamba na timu za Simba na Yanga.

Tabora inayocheza Ligi Kuu kwa msimu wa pili, imemleta kocha Anicet Kiazayidi kutoka DR Congo  aliyewahi kuzinoa timu kadhaa za nchini kwao ikiwamo AS Maniema Union iliyowahi kutumikiwa na Maxi Nzengeli aliyepio Yanga kwa sasa ambaye jioni ya leo ataikabili Tabora katika Ligi Kuu.

Pia amemnoa nyota mopya aliyesajiliwa hivi karibuni, Ellie Mpanzu anayesubiri dirisha dogo lifunguliwe aanze mambo na kikosi hicho cha Msimbazi, mbali na Steven Ebuela aliyepo Al Hilal ya Sudan) enzi akiinoa Maniema, lakini pia amewahi kuzifungdiosha AS Vita, AS Simba na Les Aigles du Congo.

Tabora imemnyakua kocha huyo kuchukua nafasi ya Mkenya Francis Kimanzi aliuefungashiwa vierago baada ya timu kuwa na mwenendo mbaya katika Ligi Kuu inayoiocheza baada ya kunusurika kushuka kupitia mechi za play-off dhidi ya Biashara United iliyopo Championship.

Mmoja wa viongozi wa timu hiyo, aliliambia Mwanaspoti, kwamba kocha huyo anaweza akaanza majukumu yake wakati wowote, kutokana na kukamilisha kwa asilimia kubwa taratibu zinazotakiwa.

“Ni kocha mwenye CV kubwa, hivyo tunaamini atatuvusha katika malengo yetu kwa msimu huu, kwani tunatamani kumaliza nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu,” alisema kiongozi huyo.

Tabiora itakuwa wageni wa Yanga kuanzia saa 12 jioni ya leo kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara ikiwa imetoka kushinda michezo miwili mfululizo, tangu iachane na Kimanzi, ikiichapa Pamba Jiji na Mashujaa kila moja ikiinyuka kwa bao 1-0 yote yakifungwa kwa mikwaju ya penalti na Mnigeria Morice Chukwu.

Related Posts