Rais Mwinyi aitembelea bandari ya Shaghai

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, katika mwendelezo wa ziara yake ya kikazi nchini China, leo ametembelea Bandari ya Shanghai International Port Group (SIPG) na kukutana na uongozi wa Shirika hilo ukiongozwa na Song Xiaodong.

Bandari hiyo ni kitovu muhimu cha biashara kimataifa, ikihusisha shughuli za usafirishaji, upakuaji na upakiaji wa makontena, pamoja na uhifadhi wa makontena katika bandari kavu kutoka mataifa mbalimbali. SIPG ni moja ya bandari kubwa zaidi duniani na kiungo kikuu cha usafirishaji wa mizigo kati ya Asia na mabara mengine.

Aidha , Rais Dk. Mwinyi amejionea kwa undani jinsi Bandari ya Shanghai International Port Group (SIPG) inavyoendesha shughuli zake kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence – AI). Teknolojia hiyo imewezesha bandari ya SIPG kufanikiwa katika usimamizi na uendeshaji wa shughuli zote za makontena kwa ufanisi na kuboresha huduma mbalimbali zinazotolewa bandarini humo

Katika ziara hiyo, Rais Dk. Mwinyi ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Khamis Mussa Omar, pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

 

Related Posts