Nchi za afrika ndizo zinazotajwa kuwa na mzigo mkubwa wa ongezeko la taka za kielektroniki kutokana na kutokuwa ujuzi na zana za kisasa kuzifanya taka hizo kuwa matumizi mengine mbadala.
Benki ya Dunia imeonya kuhusu kitisho kinachoendelea kuikabili dunia kutonana na ongezeko hilo la kasi na kwamba madhara yake siyo tu kwamba yale ya kiumazingira bali pia ustawi wa jamii uko hatarini kuathiriwa kiafya.
Serikali ya Tanzania kama ilivyo kwa mataifa mengine afrika inakiri kuhusu kuelemewa na mzigo wa ongezeko la taka la kielekitroniki na hatua hiyo inachangiwa na ongezeko la matumizi ya simu za mikononi, kopyuta pamoja na vifaa vingene vya umeme vinavyoingizwa kwa wingi kutoka mataifa ya ng’ambo ikiwemo Uchini na Ulaya.
Kwa mujibu kamishna wa tehama Nkundwe Mwasoga, kiwango cha taka za kielekikroniki kinachozaliwa nchini kwa mwaka kinakadiriwa kufikia tani 33,000.
SomaUlaya yalaumiwa kuigeuza Afrika dampo la taka
Anasema, jambo linalozidisha wasiwasi ni kwamba, ni asilimia tatu tu katika kiwango hicho ndicho kinachokusanywa na kugeuzwa kwa ajili ya matumizi mengine mbadala.
Benki ya dunia inasema kutokana na ukubwa wa tatizo hilo imelazimika kuanzisha mradi maalumu unaotelezwa katika nchi kadhaa za afrika ambao malengo yake ni kuwezesha taka hizo zinaondoka katika mzunguko wa kawaida.
Mtaalamu wa masuala ya mazingira kutoka Benki ya Dunia, Jane Kibasa anasema shabaha chombo hicho cha kimataifa ni kuona mataifa ya afrika yanaanza kuzimulika sera zake ni kisha kutoa kipaumbele katika sekta ambazo uzalishaji wa taka za aina hiyo ni mkubwa mno.
Ingawa wataalamu hao hawajadokeza ni kwa kiwango gani wanakusudia kupunguza kiwango cha taka hizo, lakini hata hivyo baadhi ya nchi zimeanzisha mashirikiano pamoja na taaisis za kiraia kwa ajili ya kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi.
Lawrance Nsuhu ambaye amekuwa akiendesha kampeni ya kutoa elimu pamoja na kukusanya taka ngumu za kielekitronini nchini Kenya anasema hakuna mjanja ambaye anaweza kujitapa kuwa haweizi kukubwa na athari zitokanazo na vifaa vya kielekitroniki zikizokwisha muda wake.
Afisa wa baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira(Nemc), Liliani Lukambuzi amekokeza kuhusu shabaha ya wataalamu hao kukutana pamoja akiamini kuwa ni uwanja unatoa suluhisho la kusaka mbadala wa tatizo hilo.
Baadhi ya nchi zinazoshiriki katika majadiliano hayo ya kitaalamu ni pamoja na mwenyeji Tanzania, Ghana, Zambia, Kenya na Senegal.