Watu 14 wamefariki Dunia na wengine 09 kujeruhiwa katika ajali ya gari Tabora

Watu 14 wamefariki Dunia na wengine 09 kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya Toyota Hiace yenye usajili namba T. 562 DGG baada ya dereva wa gari hiyo ambaye hajafahamika Jina kugonga fuso Mitsubishi lenye usajili namba T. 361 CSB Katika kijiji cha Mwansengo kata ya Itobo wilayani Nzega mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Richard Abwao amesema waliofariki katika ajali hiyo ni wanaume 08,Wanawake 04 na watoto 02 na majeruhi 09.

“Novemba 07,2024 majira ya saa mbili na dakika ishirini Kuna ajali imetokea katika barabara ya Itobo-Bukene katika kijiji cha Mwansengo,kata ya itobo ambapo dereva wa gari lenye namba za usajili T. 562 DGG Toyota Haice likendeshwa na dereva ambaye hajafahamika Jina alikimbia baada ya kugonga gari namba T. 361 CSB,Mitsubishi Fuso na kusababisha vifo vya watu 14 na chanzo cha ajali hii ni uzembe wa dereva ambaye alikuwa akijaribu kulipita Lori lililokuwa mbele yake na kushindwa kulimudu gari lake na kuligonga Lori upande wa kulia kwa nyuma na kuingia chini ya uvungu wa Lori.”Richard Abwao.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospital ya wilaya ya Nzega na miili 09 imetambuliwa na ndugu ikiwa majeruhi 02 wapo hospitali ya Nzega na wengine wamepatiwa Rufaa kwenda hospitali ya Nkinga.

Related Posts