Hafla ya makabidhiano ya zawadi hiyo imefanyika mapema leo, Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam ikiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo na Binafsi wa benki ya NBC Elibariki Masuke pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hiyo Bw Masuke alisema zawadi hiyo ya gari ni moja kati ya zawadi mbili za namna hiyo huku akibainisha kuwa bado kuna fursa kwa wateja zaidi kuendelea kujishindia zawadi kama hiyo pamoja na zawadi nyingine ikiwemo fedha taslimu, simu za mikononi, ‘laptops’, friji, ‘tablets’ za watoto, bima za afya pamoja na majiko ya kisasa ya kupikia.
“Leo tumekabidhi zawadi hii ya gari kwa mmoja wa mshindi wetu wakuu wa kampeni yetu ya ’Shinda mechi zako Kinamna yako’ tuliyoizindua mwezi Aprili mwaka huu, na tunatarajia kukabidhi zawadi kama hii siku chache zijazo. Ifahamike kwamba mbali na mshindi huyu, tumekuwa tukibabidhi zawadi mbalimbali kila mwezi. Tofauti na zawadi hii tayari tumeshakabidhi zawadi nyingine zenye thamani zaidi ya milioni 50 kwa washindi zaidi ya 45 waliopatikana kupitia kampeni hii,’’ alisema Masuke.
Akizungumzia zaidi kampeni hiyo inayolenga makundi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi ambao ni wateja wa benki hiyo wakiwemo wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na wanafunzi, Bw Masuke alisema inahusisha wateja wote waliokidhi vigezo na masharti na wanaohudumiwa na benki hiyo kupitia huduma zake mbalimbali zikiwemo akaunti za Chanua, Akaunti ya Malengo, Akaunti ya Mwalimu pamoja na akaunti ya Johari.
Bw Masuke aliwasihi wateja mbalimbali wa benki hiyo hususani vijana kutumia vema fursa hiyo iliyotolewa na benki ya NBC kupitia kampeni hiyo ili waweze kunufaika kupitia zawadi mbalimbali zinazoambatana na kampeni hiyo.
“Tunaposema shinda mechi zako kupitia kampeni hii tunalenga kuitumia falsafa ya mchezo wa soka ambao Benki ya NBC ndio wadhamini wakuu wa ligi tatu muhimu hapa nchini ikiwemo Ligi ya Kuu ya NBC. Tunaingiza falsafa hiyo kwenye maisha tukiamini kwamba wateja wetu wana ndoto, malengo na maazimio mbalimbali waliyopanga kufanikisha hususani kiuchumi na kijamii ikiwemo ujenzi, kukuza biashara zao, kusomesha watoto na mengine mengi…kupitia kampeni hii tunalenga kuwasaidia kufanikisha hilo,’’ alisema.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake, Bw Massana pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa makabidhiano hayo alisema amekuwa mteja wa muda mrefu wa benki hiyo kutokana na kuridhishwa kwake na huduma zinatolewa na benki hiyo ikiwemo huduma ya miamala ya kifedha na mikopo mbalimbali.
“Nimekuwa mteja wa muda mrefu wa benki ya NBC, na kila wakati nikiangazia huduma zao nahamasika zaidi kuendelea kuhudumiwa na benki hii. Wafanyakazi wa benki hii wameonyesha kujitolea kwa wateja kupitia utoaji wa huduma bora na kwa weledi wa hali ya juu. Zawadi hii si tu gari, bali ni alama ya matumaini na mafanikio kwangu.’’
“Nitatumia usafiri huu kwa matumizi ya familia yangu, kutafuta fursa mpya, na pia kukuza biashara yangu. Kupitia zawadi hii mimi ni kama mwanga wa matumaini kwa wateja wengine wa benki hii, kwamba kila mmoja ana nafasi yake ya kushinda.’’ Alisema.
Mkurugenzi wa Idara ya Wateja wadogo na Binafsi wa benki ya NBC Elibariki Masuke (Katikati) akimpongeza Bw Massana Gibril (Kulia) mkazi wa jijini Arusha alieibuka mshindi wa zawadi kuu ya gari aina aina BMW X1 kupitia kampeni ya ’Shinda mechi zako Kinamna yako’ inayoendeshwa na benki hiyo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya zawadi hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Anaeshuhudia ni Mdhibiti Fedha wa benki hiyo Bi Veronica Kanyama (kushoto)
Mdhibiti Fedha wa benki ya NBC Bi Veronica Kanyama (kulia) akikabidhi ufunguo wa gari kwa Bw Massana Gibril (katikati) mkazi wa jijini Arusha alieibuka mshindi wa zawadi kuu ya gari aina aina BMW X1 kupitia kampeni ya ’Shinda mechi zako Kinamna yako’ inayoendeshwa na benki hiyo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya zawadi hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wateja wadogo na Binafsi wa benki ya NBC Elibariki Masuke (kushoto)
“Nitatumia usafiri huu kwa matumizi ya familia yangu, kutafuta fursa mpya, na pia kukuza biashara yangu. Kupitia zawadi hii mimi ni kama mwanga wa matumaini kwa wateja wengine wa benki hii, kwamba kila mmoja ana nafasi yake ya kushinda.’’ – Bw Massana Gibril (katikati) mshindi wa ya gari aina aina BMW X1 ambayo ni zawadi kuu ya kampeni ya ’Shinda mechi zako Kinamna yako’ inayoendeshwa na benki ya NBC.
Bw Massana Gibril (alieketi ndani ya gari) ambae ni mshindi wa ya gari aina aina BMW X1 ambayo ni zawadi kuu ya kampeni ya ’Shinda mechi zako Kinamna yako’ inayoendeshwa na benki ya NBC akijaribu ubora wa gari hiyo mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo. Kushoto ni Mdhibiti Fedha wa benki ya NBC Bi Veronica Kanyama
Muonekano wa gari aina BMW X1 ambayo ni zawadi kuu ya kampeni ya ’Shinda mechi zako Kinamna yako’ inayoendeshwa na benki ya NBC.