Gamondi achomoa kikao cha mabosi Yanga

Wakati mabosi wa Yanga wakitawanyika kuashiria kumalizika kikao kizito kilichobeba ajenda za matokeo ya timu hiyo usiku wa kuamkia leo, taarifa zinasema kocha wa kikosi hicho, Miguel Gamondi hakuhudhuria.

Yanga jana ilipoteza mchezo wa pili mfululizo wa Ligi Kuu Bara mbele ya Tabora United kwa mabao 3-1, baada ya wiki iliyopita kufungwa kwa bao 1-0 na Azam FC katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na kocha huyo zinasema Gamondi alipokea wito wa kikao hicho, lakini akaomba udhuru kwamba atawaona leo viongozi wake.

Hata hivyo, udhuru ya Gamondi haukuzuia kikao hicho kuendelea ambapo mabosi hao walijifungia na kujadili mambo mazito kuhusu kiwango cha timu yao.

Mwanaspoti inafanamu kwamba Yanga huenda ikachukua uamuzi mzito.

Related Posts