KAMPUNI YA SHANXI YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO DIT

 

KAMPUNI ya ujenzi ya Shanxi imekabidhi vifaa vya michezo kwa uongozi wa wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) ikiwa ni muendelezo wa kuhamasisha michezo kwa wanafunzi.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya Sh milioni 25 kwa Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi,  Meneja Mradi wa kampuni hiyo, William Zang amesema vifaa hivyo ni sehemu ya kampuni hii kurejesha katika jamii kwa lengo la kuwaweka pamoja vijana na kuwawezesha kufanikisha maandalizi ya michezo yao.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi, Mboje Richard Busia ameushukuru uongozi wa Kampuni kwa vifaa hivyo vya michezo. 

“Tunashukuru sana kwa vifaaa hivi kulikuwa na uhaba wa vifaa vya michezo kwa michezobyote na kampuni hii imetuwezesha ambavyo vitatufaa tunapoelekea kwenye michezo yetu ya SHIMIVUTA” amesema.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Wanafunzi wa Taasisi, Josia Heziron Mnzava ameushukuru uongozi wa Shanxi kwa kufanikisha hili na kwa kuwa vifaa hivi vitasaidi kuongeza ushiriki wa wanafunzi katika michezo hasa mashindano ya vyuo vikuu

Related Posts