Mafuru afariki dunia, Rais Samia aomboleza

Dar es Salaam. Aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Mafuru amefariki dunia leo Jumamosi Novemba 9, 2024 katika Hospitali ya Apollo nchini India.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameomboleza kifo cha mafuru akitoa pole kwa familia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji).

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kilichotokea leo Novemba 9, 2024 katika hospitali ya Apollo nchini India.

“Ninatoa pole kwa familia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Alexander Mkumbo, watumishi wa Tume ya Mipango, ndugu jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.”

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts