MZUMBE NA KHUNE FOUNDATION YAWAPIGA MSASA WATAALAM UGAVI NA UNUNUZI KUKUTANA TENA NOVEMBA 27, 2024

Mratibu wa Mradi wa  Khune Foundation, Profesa Omary Swalehe akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya masuala ya ugavi na usafirishaji, mafunzo hayo yamefanyika Chuo Kikuu Mzumbe jijini Dar es Salaam.

Matukio mbalimbali wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku tatu yaliyofanyika chuo Kikuu Mzumbe jijini Dar es Saalam.

Mratibu wa Mradi unaofadhiriwa na  Khune Foundation, Profesa Omary Swalehe akigawa vyeti kwa waliohudhulia mafunzo ya Ugavi na Usafirishaji yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Khune Foundation imewajengea uwezo Wataalamu wa Ununuzi, Ugavi na Usafirishaji kutoka sekta binafsi  pamoja na watumishi wa umma  kuhusu usimamizi wa mikataba kwenye mnyororo wa ununuzi na ugavi.

Hatua hiyo imekuja baada ya kubaini changamoto katika taarifa mbalimbali ikiwemo Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi na Ugavi (PPRA) katika eneo la usimamizi wa miktaba hali sio nzuri kwani fedha nyingi zinapotea kutokana na wasimamizi kutokuwa na uwelewa mkubwa.

Akizungumza leo Novemba 08, 2024 Jijijni Dar es Salaam wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu, Mratibu wa Mradi unaofadhiriwa na  Khune Foundation, Profesa Omary Swalehe amesema kuwa wataalam wa ununuzi na ugavi zaidi 65, wamepata mafunzo hayo katika maeneo mhimu ya ununuzi na ugavi.

Prof. Swalehe amesema kuwa katika bajeti nchi, serikali imekua ikitumia fedha nyingi katika ununuzi, ugavi na usafirishaji ili kuhakikisha jamii inapata huduma stahiki. 

Kwa Upande wa Mshiriki wa mafunzo hayo ambaye ni Afisa Manunuzi wa kutoka chuo Hospitali ya Muhimbili, Melkiory Sallema amesema kuwa  mafunzo waliyoyapata yatawasaidia kwa kwenda kutoa ujuzi huo kwa maafisa Manunuzi wengine ili kuwa na uelewa wa pamoja.

Amesema kuwa wamejua namna mikataba ya manunuzi inavyotengenezwa pamoja na kujua maudhui ya mikataba hiyo  inavyosimamiwa kuanzia mkataba unavyoanza kuundwa.

Pia amesema kuwa wamepata mafunzo ya namna ya kukabiliana na migogoro kati ya pande mbili zikitofautiana kati ya mtoa huduma na mpokea huduma.

Kupitia mafunzo haya tunaenda kupeleka ujuzi mpya wa usimamizi ya mikataba ya manunuzi.

Afisa Manunuzi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Morogoro, Eva Sichome amesema kuwa mwanzoni walikuwa wakifanya kazi kwa mazoea sasa wamepata mafunzo ya namna ya kusimamia, kutatua migogoro pamoja na kutekeleza masuala mazima ya Manunuzi na ugavi katika taasisi zetu.

Amesema kwa sasa watatekeleza majukumu yao kwa weledi zaidi kutokana na taaluma waliyoipata kwa ufadhili wa Khune Foundation unaosimamiwa na Chuo Kikuu Mzumbe.

Related Posts