Wagosi kutesti mbili Kenya | Mwanaspoti

COASTAL Union imesema huenda ikacheza michezo miwili ya kirafiki itakapokwenda Kenya kwa mapumziko ya wiki mbili ya kusimama kwa Ligi Kuu Bara kupisha kalenda ya michuano ya kimataifa kwa timu za taifa.

Wagosi wa Kaya inayonolewa kwa sasa na kocha Juma Mwambusi imeshacheza mechi 10 za ligi na kushinda mitatu, sare tatu na kupoteza michezo mitano ikiwa nafasi ya 10 katika msimamo unaoongozwa na Simba kwa sasa yenye pointi 25 kwa idadi kama hiyo ya mechi mbele ya Yanga yenye 24 na Singida BS yenye 23. Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Habari wa Coastal, Abbas El-sabri alisema kama timu wamefikiria kucheza mechi mbili za kirafiki kwa timu ambazo hazishiriki ligi kuu.

El Sabri alisema hadi leo jana jioni wangeshafahamu ni timu zipi za mjini Mombasa Kenya watazocheza nazo kutokana na urahisi wa usafiri.

“Kama kila kitu kitaenda sawa hadi Jumatatu hii tunaweza kuanza safari ya kwenda Mombasa, kutokana na likizo ndefu tunahitaji kuendelea kuwa fiti ili ikirejea tuendelee tulipoishia,” alisema El Sabri na kuongeza

“Kikosi chetu kiko mikono salama chini ya kocha Mwambusi mechi tano za mwanzo hatukuanza vizuri lakini sasa kikosi angalau kimeanza kuleta matumaini kuelekea malengo yetu ya kumaliza nafasi nne za juu.”

Related Posts