09/11/2024 DAR ES SAALAAM
Askari Polisi wanaoendela na mafunzo ya upandishwaji vyeo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam wametakiwa kuzingatia kile wanachofundishwa ili kwenda kutoa huduma bora kwa wananchi pamoja na askari watakaoenda kuwasimamia pia Kwenda kukabiliana na uhalifu na wahalifu kwenye maeneo yao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Dkt. Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na wanafunzi wa Kozi ya Uofisa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi mara baada ya kupokea msaada wa vifaa mbalimbali vya kitaaluma vilivyotolewa na wanafunzi na kuwasisitiza kusoma kwa bidii ili kuongeza maarifa na jitihada za kutosha katika kudhibiti vitendo vya kihalifu.