Chama la Mtanzania laitandika Mamelodi CAF

CHAMA la Mtanzania, Hasnath Ubamba anayekipiga FC Masar ya Misri limeichapa Mamelodi Sundown Ladies bao 1-0 mchezo wa kwanza wa makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ubamba ambaye yupo kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Fountain Gate Princess ya Dodoma amekuwa na kiwango bora tangu ajiunge na timu hiyo.

FC Masar inashiriki michuano hiyo baada ya kuwa bingwa kwa ukanda wa UNAF ikiwa miongoni mwa timu nane zinazocheza michuano hiyo ambayo ilianza kutimua vumbi Novemba 09 nchini Morocco.

Hii inakuwa rekodi kwa timu hiyo ya Misri kuifunga Mamelodi ambao ni mabingwa mara nyingi wa michunao hiyo ikichukua 2021/22 na 2023/24.

Timu hiyo ilianza kampeni zake jana ya kutafuta ubingwa wa Afrika baada ya kuitandika Mamelodi dakika ya 45 bao lililofungwa na Sandrine Niyonkuru.

Kwenye mchezo huo Ubamba alianza kama winga na kumaliza dakika zote 90 na kupata nafasi ya kupata bao ambalo hakuweza kuukwamisha mpira wavuni.

Ndani ya dakika 90 alizocheza nyota huyo ambaye ndio mara yake ya kwanza kucheza michuano ya kimataifa alionyesha kiwango bora lakini akikosa utulivu anapokuwa kwenye lango la mabingwa hao watetezi wa CAF.

Kwa matokeo hayo yanaifanya timu hiyo ikae kileleni mwa msimamo wa kundi B ikiwa na pointi tatu, C.B.E ya Ethiopia, Edo Queens na Mamelodi ikiburuza mkiani.

Kundi A inaongoza AS Far Rabat na pointi tatu sawa na TP Mazembe iliyopo nafasi ya pili,

UWC na Aigles de la Médina ambazo ziki mkiani.

Msimu huu kwa Tanzania hakuna mshiriki baada ya Simba Queens kutolewa mapema kwenye michuano ya CECAFA ambayo C.B.E ndio mwakilishi.

Related Posts