Kisisa mambo freshi | Mwanaspoti

KIUNGO wa Yanga Princess, Irene Kisisa atarejea uwanjani hivi karibuni baada ya kutoka kwenye majeraha ya goti aliyoyapata msimu uliopita.

Mara ya mwisho nyota huyo kuonekana uwanjani ni Aprili 25, mwaka huu kwenye mchezo wa dabi dhidi ya Simba na Yanga ilipoteza kwa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kisisa alisema ameanza mazoezi na timu na ripoti inaonyesha anaendelea vizuri, hivyo muda wowote mtamuona uwanjani.

Aliongeza licha ya kukaa muda mrefu, anatamani arejee na kiwango bora ambacho kitaisaidia Yanga.

“Muda si mrefu nitarejea, nimeanza kufanya mazoezi na timu taratibu, hivyo mashabiki watusapoti naamini kama wachezaji tutapambana kwa uwezo,” alisema Kisisa.

Related Posts