Rais Samia aipa Tanroad zaidi ya Bil 500,ujenzi wa miundombinu Dar

Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan zaidi ya Shilingi Bilioni 500 zimetolewa kwa Wakala ya Barabara Tanzania-TANROADS Mkoani Dar es salaam.

Licha ya kusimamia matengenezo ya barabara na madaraja, katika kipindi cha miaka mitatu Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya Kimkakati ambayo utekelezaji wake upo kwenye hatua mbalimbali sambamba na kuhakikisha mtandao wa kilomita 619 za barabara zinazosimamiwa na TANROADS zinapitika wakati wote.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es salaam Mhandisi John Mkumbo leo tarehe 8 Novemba 2024 wakati akitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa miradi ya barabara, madaraja pamoja na vivuko katika mkoa huo.

Ameitaja miradi inayoendelea kuwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka BRT awamu ya pili (Km 20.3) inayohusisha barabara ya Kilwa; barabara ya bandari – Gerezani (Kariakoo), Barabara ya Chang’ombe toka makutano ya barabara ya Nyerere hadi Mgulani; Barabara ya Kawawa toka Magomeni hadi barabara ya Nyerere na barabara ya Sokoine toka Gerezani hadi jengo la Mwalimu Nyerere kwa gharama ya Shilingi Bilioni 260.

Ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka BRT awamu ya tatu (Km 23.3) kutoka katikati ya Jiji hadi Gongolamboto na inahusisha barabara za Azikiwe toka Posta ya Zamani hadi Maktaba; Barabara ya Bibi Titi, Barabara ya Nkurumah na barabara ya Nyerere, pia inahusisha ujenzi wa Barabara ya Uhuru kuunganisha mfumo wa usafiri kutoka kituo kikuu cha Gerezani hadi Gongolamboto kwa kupitia Buguruni kwa gharama ya Bilioni 231.

ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka BRT awamu ya nne (Km 30.1) kutoka katikati ya Jiji hadi Tegeta ambapo inahusisha barabara ya Ali Hasan Mwinyi kuanzia Maktaba hadi Tegeta pamoja na Sam Nujoma kutoka Mwenge hadi Ubungo kwa gharama ya Shilingi Bil 429

Mhandishi Mkumbo amesema mjwa pia TANROADS Mkoa wa Dar es salaam imekamilisha Utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa daraja la muda katika eneo la mto Mpiji Chini kurejesha mawasiliano kati ya Mbweni na Kiembeni baada ya daraja lililokuwepo kuathiriwa na mvua za El Nino. Huku TANROADS ikitarajia kuanza ujenzi wa daraja la kudumu la mita 140 na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 2.3

Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Dar es salaam Mhandisi Clever Akilimali amesema kuwa pamoja na ujenzi unaoendelea wa barabara ya njia nane kutoka Kimara hadi Ubungo ikijumuisha njia za mwendokasi na njia za pembeni pia kuna mradi wa uwekaji wa taa za kuvusha watembea kwa miguu.

Mhandisi Akilimali amesema kuwa katika barabara ya Kimara hadi Kibaha TANROADS imefunga jumla ya taa 560 za mwanga, sambamba na kujenga vituo vya mabasi 6, huku taa za kuongozea magari zikiwa zimefungwa tisa kwenye makutano (junction) ya barabara.

   

 

Related Posts