Ujumbe Unaosambaa juu ya M-Koba ni UZUSHI na UONGO

 

Vodacom Tanzania na Benki ya TCB wameujulisha umma na wateja wao kwamba ujumbe wa hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii unaodai kwamba huduma ya M-Koba inakaribia kufungiwa kutokana na madai ya madeni yasiolipwa kwa Serikali ni wa uongo na uzushi unaokusudia kuleta taharuki kwenye jamii.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Vodacom na Benki ya TCB wawahakikishia wateja wao wote wa M-Koba kwamba akaunti zao ziko salama na zinafanya kazi kama kawaida.

Vodacom na Benki ya TCB pia wamewahakikishia wateja wa M-Koba kwamba usalama wa wateja na usalama wa akaunti zao ni kipaumbele chake cha juu na wanatumia njia madhubuti za kulinda faragha ya wateja na kudumisha uaminifu wa huduma zao za kifedha

Umma unashauriwa kupuuza habari za uongo na kutegemea njia rasmi za Vodacom kwa taarifa za uhakika. Vodacom pia inafanya kazi kwa karibu na mamlaka husika ili kubaini chanzo cha habari hizi za uongo na kuchukua hatua zinazostahili.

Huduma ya M-Koba inaletwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya TCB chini ya usimamizi wa Benki kuu ya Tanzania (BOT).

Related Posts