Jonathan Budju afunga mwaka na ‘My Savior’

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mwimbaji nyota kutoka nchini Canada, Jonathan Budju, amewataka mashabiki wa muziki huo kukaa tayari kwa ujio wa ngoma mpya, My Savior itakayotoa mwishoni mwa wiki hii.

Jonathan Budju ambaye ni miongoni mwa waimbaji wachache wa Diaspora wanaofanya vizuri Afrika Mashariki kupitia nyimbo kama Tawala, Utukufu, Ngolu na nyingine zenye namba kubwa mtandaoni.

Akizungumza na mtanzania.co.tz, Budju amesema mapema Ijumaa hii ataachia audio ya wimbo My Savior na wiki moja mbele atatoa video yake.

“Wimbo huu ni ‘my testimony’ (ushuhuda wangu), unazungumzia maisha yangu na Mungu, ninaamini utagusa maisha ya wengi hivyo wapenzi wa huduma yangu wakae tayari kubarikiwa,” amesema Budju a.k.a Son of God.

Related Posts