Aweso Aitaka Sekta ya Maji Kunufaika na Utafiti wa Chuo cha Maji

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amezitaka taasisi za Sekta ya Maji kukitumia Chuo cha Maji katika kupata majibu changamoto zinazojitokeza katika huduma ya maji nchini.

Aweso amesema hayo katika mahafali ya 48 ya Chuo cha Maji jijini Dar es salaam ambapo wahitimu 684 wamehitimu.

Amesema Chuo cha Maji moja ya lengo lake ni kufanya tafiti zinazohusu Sekta ya Maji.

Moja ya ubunifu wa chuo hicho ni teknolojia ya kubaini mivujo katika mabomba ambayo inaweza kutumika katika mamlaka za maji. Hivyo, teknolojia itumike kuleta mageuzi zaidi katika huduma ya maji.

Aweso amesema mageuzi makubwa yamefanyika ili kukifanya chuo hicho kuwa bora zaidi, ikiwamo miundombinu ya majengo na matokeo mazuri yanaonekana.

Waziri Aweso ameainisha kuwa Tanzania imeongoza kwa miaka miwili mfululizo kati ya nchi 40 katika ujenzi wa miradi ya maji na kutambuliwa na Benki ya Dunia.

Ameelekeza wahitimu wa Chuo cha Maji kutumika katika usimamizi na uendelevu wa miradi ya maji nchini.

Aweso amesema ili Taifa liendelee linahitaji nguvu kazi. Awewataka wahitimu kuzingatia nidhamu, uadilifu na uzalendo kwa dhati ili kufikia viwango vya juu.











Related Posts