Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

 


Meneja Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Hance Mapunda (kushoto), Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa, Bi. Abigail Lukuvi ( wa pili kushoto) , Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian Thomas, Mkuu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Bi. Sezaria Kiwango na Meneja Rasilimali Watu mwingine wa benki hiyo, Bi. Anna Chacha wakishangilia baada ya kuzindua kisima kilichojengwa na wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi ( wa pili kushoto) , Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian Thomas na Mkuu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Sezaria Kiwango wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kisima kilichojengwa na wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Ni mwendelezo wa wafanyakazi wa benki hiyo kufanya huduma za kijamii katika shule hiyo Kwa takriban miaka mitatu sasa. Kutoka Kushoto ni Mameneja Rasilimali Watu wa benki hiyo, Bw. Hance Mapunda na  Bi. Anna Chacha.

Mkuu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Bi. Sezaria Kiwango (kulia), akikabidhi cheti cha shukurani kwa maofisa wa Benki ya Absa Tanzania, mara baada ya kupokea msaada wa kisima Cha maji kilichojengwa na wafanyakazi hao, katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Dar es Salaam jana. 

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi ( kushoto) akikabidhi kisima kilichojengwa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Nabili Tuli jijini Dar ea Salaam jana.

Related Posts