Hekari 100 zateketea kwa moto Arumeru

Hekari zinazokadiriwa kufikia zaidi ya mia moja zimeteketea kwa moto katika mashamba ya Dolli Estate yanayomilikiwa na baadhi ya wawekezaji kutoka nje katika kata ya Maroroni Wlayani Arumeru Mkoani Arusha huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika

Moto huo ambao umewaka kwa zaidi ya saa sita umeunguza mashamba hayo jambo lililofanya helkopta kutumika kwa lengo la kuangalia uharibifu huo uliotokea

Raia wa nje ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema “sijui ilianza wapi niliona mapema kidogo halafu nikafanya alarm kwenye group nikaita watu njoo nisaidie watu wamekuja kutoka kila mahali,tumshukuru Mungu wamekuja watu kunisaidia”

Hadi hivi sasa hakuna tathimini yeyote iliyotoleea na serikali kuhusu madhara yaliyotokea lakini tutaendea kufuatilia ili kupata taarifa zaidi

Related Posts