Mbaroni kwa madai ya kumtukana Rais Museveni

Wananchi wawili nchini Uganda wamewekwa rumande kwa tuhuma za kumtukana Rais Yoweri Museveni, mkewe  Janet Museveni na mtoto wake Jenerali Muhoozi Kainerugaba.

Watu hao wanadaiwa kutenda kosa hilo hivi karibuni kwa kutumia mtandao wa Tiktok.

Watuhumiwa hao  ni David Ssengozi  anayejulikana kwa jina la Lucy Choice (21) na Isaiah Ssekagiri (28) walifikishwa mbele ya Hakimu Stella Amabillis ambaye aliamuru jana Novemba 12, 2024 wapelekwe mahabusu ya Gereza la Kigo hadi kesi yao itakapoitwa kwa ajili ya kusikilizwa mahakamani leo Novemba 13, 2024.

Watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya kutoa lugha chafu na kusambaza taarifa za uongo dhidi ya Rais na familia yake.

Awali, mwendesha mashitaka alisema maudhui yaliyokuwa yametumwa mtandao wa Tiktok yalilenga kuichafua familia ya kiongozi huyo.

Related Posts